AVAA SUTI ILIYOLOA HEDHI KUSHINIKIZA SHERIA, AFUKUZWA BUNGENI
Gloria Orwoba ambaye ni mbunge wa muungano unaotawala nchini Kenya, amefukuzwa bungeni baada ya kuingia akiwa na suti nyeupe, yenye madoa ya damu, yanayoaminika kuwa ni hedhi, ili kushinikiza uwepo wa sheria ya kutoa taulo zakike bure kwa watoto mashuleni.
Maseneta walikatiza kikao cha bunge, wakimtaka spika kumtoa mbunge huyo kwa kuwa alivaa mavazi yasiyofaa.
Spika alimtaka mbunge huyo kutoka nje na kubadilisha mavazi yake ndipo arejee, lakini akiwa nje ya ukumbi wa bunge, aliwaambia waandishi wahabari kuwa anafanya hivyo kama shinikizo la kutaka taulo hizo za kike zitolewe kisheria kwa watoto wa kike mashuleni.

Post a Comment