UWANJA WA BENJAMIN MKAPA KUFUNGIWA NA CAF
Shirikisho la Soka Barani Africa CAF, limeufungia Uwanja wa Benjamin Mkapa wa jijini Dar es Salaam kwa kile ilichosema kukosa vigezo.
Taarifa ikuyotolewa na CAF, yenye makao yake nchini Misri,imesema sehemu ya kuchezea ya uwanja huo yaani pitch imekosa ubora kutokana na uwanja huo kutumika mara kwa mara.
Limesema ili kulinda ubora wa sehemu hiyo ya kuchezea, uwanja huo unapaswa kutumika si zaidi ya mara tatu kwa wiki, lakini wenyewe umekuwa ukitumika hadi mara nne kwa wiki.
Kwa ajili hiyo, uwanja huo utafungiwa kwa muda wa mwezi mmoja ili urejee katika ubora wake.
Uwanja huo unatumiwa na timu za Simba na Yanga zinazoshuriki michuano ya vilabu barani Afrika.

Post a Comment