UJENZI BOMBA LA MAFUTA SASA RUKSA

Serikali imetoa kibali ili kuruhusu ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kipande cha Tannzania, kinachoanzia Mtukura mkoani Kagera hadi Chongoraeni mkoa wa Tanga.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba, wakati akikabidhi kibali cha ujenzi huo kwa kampuni ya EACOP, aliitaka Mamlaka ya Nishati na Maji Ewura, kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kufiikia malengo yaliyokusudiwa.

Bomba hilo linalotokea Uganda, litapita katika mikoa ya Kagera, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara hadi Tanga.

No comments