UKIKAMATWA KWA USHOGA UGANDA UTAFIA JELA
Wakati dunia ya wazungu ikisisitiza haki za binadamu, kwa kusema mapenzi ya jinsia moja ni haki ya wahusika, nchini Uganda, Rais Yoweri Museveni ameweka wazi kuwa mtu yeyote atakayekamatwa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Yoweri, mmoja wa viongozi walikaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, amesema ndoa za jinsia moja hazikubaliki nchini kwake.
Siku chache zikizopiga, Museveni alishangaaa wanaume wanaowafuata wanaume wenzao na kuwataka kimapenzi, akisema wingi wa warembo unampa wasiwasi kuwa mwanaume huyo hayuko sawa akilini mwake.
Nchi kadhaa za Afrika, pamoja na mapenzi ya jinsia moja kuwa nje ya tamaduni zake, lakini zimeshindwa kutoa kauli kama za Museveni, zikiogopa kunyimwa misaada kwa kile kinachoonekana kukiuka haki za binadamu.

Post a Comment