KITWAGWA ATAKA WEZI WASIWEKEZE NJE YA NCHI
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga amewashauri wezi wa mali ya umma kuwekeza nchini.
Kitwanga ambaye katika siku za karibuni amekuwa mkosoaji wa mambo mengi, alitoa kauli hiyo wakati akishangaa taarifa za kivuko cha MV Magogoni kwenda kufanyiwa ukarabati mjini Mombasa nchini Kenya.
Kivuko hicho kilichonunuliwa kwa shilingi bilioni 9 mwaka 2008, kinafanyiwa ukarabati kwa kiasi cha shilingi bilioni 7.5 amvazo zimepigiwa kelele na wadau.

Post a Comment