MESSI MWANASOKA BORA WA DUNIA WA FIFA 2022

Mshambuliaji nyota wa timu ya soka ya PSG ya Ufaransa na timu ya taifa ya Argentina,Lionel Messi ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka na Shirikisho la soka duniani, FIFA.

Messi, aliyeiongoza Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka huu huko Qatar, alimshinda Kilian  Mbappe anayecheza naye timu moja ya PSG pamoja na mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema.

Tuzo hiyo iliambatana na kuteuliwa kwake katika kikosi bora cha mwaka kwa mara ya 16, hivyo kuwa binadamu pekee kufikisha idadi hiyo, akifuatiwa na mpinzani wake wa miaka yote, Cristiano Ronaldo aliyeteuliwa mara 15.

Hii pia ni tuzo yake ya sita ya mwanasoka bora wa mwaka wa FIFA,ambayo ni tofauti na Bor Odour.

No comments