MTOTO ALIYEZALIWA TETEMEKO LIKITOKEA SYRIA NA MAMA YAKE KUFARIKI, AASILIWA
Miujiza haiishi. Mtoto mchanga, aliyezaliwa siku tetemeko la ardhi likitokea nchini Syria, ambaye mama yake na familia yake yote walikufa, hatimaye ameasiliwa na shangaza yake.
Imeelezwa kuwa mama wa mtoto huyo alipatwa na uchungu wakati tetemeko hilo likitokea na akajifungua wakati ghorofa wanaloishi lilipoporomoka, hata hivyo alifanikiwa kujiokoa na kutoka chini ya kifusi akiwa bado hajatenganishwa na kitovu na mtoto wake.
Baada ya kufikishwa hospitalini alifariki baadae lakini mtoto huyo ni mwenye afya njema na jana shangazi yake alimuasili na kumtangaza kama mwanae.

Post a Comment