TUNAWAHARIBU WENYEWE HALAFU TUSIVYO NA HOFU YA MUNGU, TUNAWALAUMU
Kuna mjadala mkubwa miongoni mwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla juu ya kushuka kwa maadili miongoni mwa watoto wa zama hizi za dotcom.
Watoto wa zama hizi (2000+), hawaonekani kujali, kulinda wala kuheshimu kile tunasema maadili ya Kitanzania, ambayo kimsingi ni pamoja na tamaduni, mila na desturi za Watanzania.
Pamoja na wingi wa makabila (Tanzania ina makabila 120+) lakini tokea enzi, wamefanikiwa kuulinda, kuutetea na kuuenzi utamaduni wao.
Lakini ghafla, mwanzoni mwa karne ya 21, vijana wameuona utamaduni ni kama kitu cha kizamani, ambacho hakiendani na hali halisi kutokanana utandawazi.
Wakati wazazi wa zama hizi wakilaumu vijana kubadilika, wanasahau kuwa wao ndiyo chanzo kikubwa.
Enzi zile nikiwa mtoto ( Early 70's) ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kupelekwa kijiji cha wazazi wako (bahati mbaya pia wazazi walioana toka koo za jirani) ili ujifunze lugha, utamaduni, maadili na desturi za ukoo, jamiii na watu wa karibu.
Tulisoma shule zile za kutembea masaa matatu kwa mguu kwenda na kurudi. Tukajuana halafu baadaye tukaletwa mijini kwa wazazi wetu tujifunze ya dunia.
Leo hiii, ni mzazi gani wa zama hizi anampeleka mtoto wake kijijinikwao ambako hakuna umeme, hakuna usafiri wala shule bora? Hatutaki kuwapeleka kwa sababu tunaamini tutawapoteza, tunataka tuishi nao ili tuwape elimu bora!!
Tunawapeleka International schools, wanafundishwa kiingereza na utamaduni wa kisasa. Mtoto akirudi shuleni, akitusalimia Hi Daddy, tunamuona ana akili!!!?
Lakini hatufahamu mengine anayokutana nayo huko. Ushoga, desturi za wazungu ndiyo wanayofundishwa huko.
Badala ya umpeleke mtoto wako wa miaka mitano akaishi na mama yako kijijini, unaona bora umpeleke boarding akanywe uji na chai!
Wala tusitafute wachawi, hebu jiulize, mwanao anajua lugha yako ya asili? Ofcoz anajua kiingereza na kifaransa, je anajua maisha ya kijadi ya jamii yako?

Post a Comment