MBOWE AMVUA NGUO DAVID SILINDE KWAO
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, amemvua nguo aliyewahi kuwa Mbunge wa chama hicho jimbo la Momba, David Silinde, akisema waliwahi kumnunulia nguo na viatu ili aweze kuwatumikia watu.
Mbowe alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jana huko Tunduma, akisema pamoja na wema huo, bado Silinde aliwasaliti wananchi waliompa ubunge na kujiunga na wale aliosema waliwatesa wananchi kwa kuwapiga, kuwajeruhi na kuwafunga.
David Silinde ni miongoni mwa viongozi kadhaa wa Chadema ambao walikihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa uongozi wa Rais John Magufuli katika kile kilichokuwa maarufu enzi hizo kama kuunga mkono juhudi za maendeleo zilizokuwa zikifanywa na serikali ya awamu ya tano.

Post a Comment