MKE WA RAIS WA MAREKANI AWASILI KENYA KWA ZIARA YA SIKU TATU
Jill Biden, mke wa Rais wa Marekani Joe Biden, amewasili na kupokelewa na mwenyeji wake, Rachel Ruto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo.
Jilll, ambaye hii ni ziara yake ya sita barani Afrika, ya tatu nchini Kenya lakini ikiwa ya kwanza akiwa First Lady,amewasili Nairobi akitokea Namibia ambako alifanya ziara ya siku mbili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili, lakini pia ikilenga kuwawezesha kiuchumi akinamama.
Alitua katika JKIA saa kumi na nusu jioni leo hii kwa saa za Afrika Mashariki, akiwa ndani ya ndege iitwayo Executive One Foxtrot (EXECIF) ambayo hutumiwa na wake wa marais wa Marekani maarufu kama FLOTUS (First Lady Of Unitad States of America).

Post a Comment