TANZANIA KUJENGA SPORTS ARENA KAWE
Tanzania itajenga kituo cha kimataifa cha michezo na burudani za ndani, Sports Arena katika mwaka huu, ambacho kitapatikana maeneo ya Kawe, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewaambia waandishi wa habari muda mfupi kabla hajahamishwa kutoka wizara hiyo kuwa tayari wamepata eneo la ekari zaidi ya 20, ambalo ukumbi wenye uwezo wakuchukua mashabiki 16,000 utajengwa.
Amesema michoro ya mradi huo imekamilika na muda wowote kuanzia mwezi ujao, ujenzi utaanza na utakamilika kati ya miezi nane hadi kumi.
Alisema hiyo ni kufuatia azma ya Rais Samia kuhakikisha Tanzania inakua na kituo kama hicho kwani lengo lake ni kuiwezesha sekta ya burudani kuwa chanzo cha mapato ya taifa.
Sports Arena kubwa zaidi barani Afrika ipo nchni Senegal ikiwa na uwezo wa kuingiza watu 15,000 kwa mara moja.

Post a Comment