RAIS SAMIA AWAHAMISHA MAWAZIRI WAWILI,MAKATIBU WAKUU WAWILI

Rais Samia Suluhu Hassan amewabadilisha mawaziri wawili katika wizara, kufuatia uteuzi ulioufanya leo.

Rais amemuhamisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed  Mchengerwa kwa kumpeleka katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dokta Pindi Chana amehamishiwa katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Pia Rais amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas kushika nafasi hiyo katika wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, Zuhuru Yunus, Saidi Yakub ameteuliwa kushika nafasi ya Abbas katika wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.


No comments