BINTI WA KAZI AUAWA NA BOSI WAKE TABATA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Debora Mabiligimba amethibitisha kifo cha msichana wa kazi kilichotokana na kuuawa huko Tabata, jijini Dar.
Mtu anayesadikika kushiriki mauaji hayo ni bosi wa binti huyo, ambaye pia ni mwanamke, ambaye aliita teksi za mitandaoni, iliyobeba mwili huo hadi hospitalini Muhimbili.
Akiwa hospitalini hapo, bosi huyo aluwaambia wahudumu wa afya kuwa binti huyo aliinyonga, lakini baada ya kuufanyia uchunguzi mwili huo, hakukuwa na dalili za kujinyonga.
Bosi wa marehemu alitoweka pasipo kujulikana, lakini wakati akiendelea kutafutwa, dereva wa teksi hiyo anashikiliwana Polisi ili kusaidia uchunguzi.
Inadaiwa bosi huyo wakati akiita teksi hiyo alitumia jina na namba ya simuisiyo yake.

Post a Comment