SIMBA, YANGA ZAREJESHWA UWANJA WA UHURU
Kufuatia kufungiwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kukikofanywa na Shirikisho la Soka Afrika, klabu mbili za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa, sasa zimerejeshwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Kabla ya ujenzi wa uwanja huu wa kisssa, kwa miaka yote mahasimu hao wa soka la nyumbani waliutumia Uwanja wa Taifa (Uhuru) kama uwanja wao wa nyumbani.
CAF imeufungia uwanja huo kwa sababu ya kuharibika kwa sehemu ya kuchezea, maarufu kama pitch.
Wikiendi hiii, Simba itasafiri kuelekea Uganda wakati Yanga ikipaa kwenda Mali kwa ajili ya mechi zao za tatu za michuano ya Ligi ya Mabingwa (Simba) na Kombe la Shirikisho wanaloshiriki Yanga.

Post a Comment