LUKAKU AMJIBU BOSI WA INTER ALIYEMKEBEHI

Romelu Lukaku, mshambuliaji raia wa Ubelgiji, amemjibu kwa vitendo bosi wake wa klabu ya Inter Milan, aliyemkebehi kabla ya mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya jana Jumatano.

Beppe Morata, Afisa Mtendaji Mkuu wa Inter, kabla ya mchezo dhidi ya FC Porto ya Ureno, alisema Lukaku amekuwa mnene kupita kiasi hivyo anapoteza ubora wake uwanjani.

Lakini Lukaku, ambaye amekuwa na msimu mbaya tangu wakati wa fainali za kombe la dunia, alimjibu kwa kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Porto,alipoingia saa moja baada ya mchezo kuanza kuchukua nafasi ya Eden Dzeko.

No comments