SAMIA AMEIRAHISISHIA KAZI CCM- INJINIA MADUNDO

Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga, Injinia Angelo Madundo, amewaambia wanachama wake kuwa Mwenyekiti wa Taifa, Rais Samia Suluhu Hasssan amewarahisishia kazi, kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.

Injinia Angelo Madundo alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, mbele ya wanachama walioongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya, Joseph Augustive Mdaka, Madundo alisema miradi mingi na mikubwa imeshatekelezwa hadi sasa, hasa katika sekta za afya, elimu na miundombinu.



 Alisema tofauti na enzi zile, katika kipindi hiki cha uongozi wa Dokta Samia Suluhu Hassan, badala ya watoto wa shule kukacha kwenda shuleni kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarasa, madawati na vyoo, jambo hilo sasa ni historia, kwani kuna madarasa ya kutosha na ya kisasa yamejengwa kiasi kwamba sasa shule ndizo zinatafuta wanafunzi.



Wengine waliotoa neno katika mkutano huo mkubwa ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya aliyemwakilisha DC, Mwanaidi aliyesema kuna mshikamano uliotukuka kati ya serikali na chama kiasi cha kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Desderius Haule alisema wao kama halmashauri, wanaendelea kuratibu na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kwenda sambamba na Ilani ya CCM.



No comments