TANESCO MBINGA SASA KIDIGITALI, NDANI YA WIKI UMEME UNAWAKA

Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, Tanesco Wilaya ya Mbinga, linatumia njia za kisasa katika utoaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini na vijijini, likisema ndani ya siku saba toka mteja aombe kuunganishiwa, umeme unakuwa umeshaingia ndani mwake.

Meneja wa Tanesco Mbinga, Malima Henzron Zabron, ameiambia Ojuku Blog kuwa wamefungua ofisi katika Kata Tano ambazo zinawahudumia wateja kwa haraka na Uhakika.


Alizitaja Kata zenye ofisi hizo kuwa ni  Luanda, Kigonsera, Litembo, Nyoni na Maguu ambazo zinawahudumia wateja wa vijiji vinavyowazunguka. Alisema ofisi hizo zina zana kamili kukabiliana na changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.

Alisema endapo tatizo lolote linajitokeza, wateja wanatakiwa kuwasiliana na ofisi hizo zilizo karibu yao ili wahudumiwe.



Kuhusu wateja wapya wanaoomba kuunganishiwa umeme, alisema hivi sasa wana mfumo mpya uitwao Nikonekt unaomsaidia mteja kuomba kuunganishiwa kidigitali badala ya kujaza fomu na kuzipeleka ofisino.

Mteja anajaza maombi online, anapokea maelekezo kielektroniki na kazi hiyo inakamilika ndani ya siku saba tu.

Kuhusu umeme vijijini, Zabron alisema hadi sasa vijiji 8 vimefikiwa na umeme wa REA, kazi inayofanywa na mkandarasi NAMIC COOPARATES LTD, ambaye hata hivyo kasi yake ilipunguzwa na uwepo wa janga la Corona.

No comments