CCM MBINGA YAADHIMISHA MIAKA 46 KATA YA LANGIRO

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga leo Jumamosi kimeadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwake katika Kata ya Langiro, ambako ilifanya shughuli mbalimbali za kijamii na hotuba.

Mwenyekiti wa CCM wilaya, ndugu Mdaka aliwaongoza viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika kukagua miradi ya maendeleo, sambamba na kuzindua kampeni ya upandaji miti.



Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya chama hicho Kata ya Langiro, Mdaka aliwataka wanachama hao kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

Alisema Rais Samia anafanya kazi nzuri katika kuiendeleza nchi, ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa shule, zahanati, barabara na miundombinu mingine muhimu.



Baadhi ya wanachama wakiburudika wakati wa sherehe hizo.



Ngoma maarufu ya Mganda ikitumbuiza wakati wa sherehe hizo.



Chifu wa Langiro, Howahowa Komba akitoa neno wakati wa sherehe hizo.




No comments