RUSSIA YASITISHA MKATABA WA SILAHA ZA NYUKLIA, YAFIKIRIA KUZIFANYIA MAJARIBIO

Russia jana ilitangaza rasmi kusitisha utekelezaji wa Mkataba wa Start, kuhusu silaha za Nyuklia na kusema wazi kuwa inaangalia uwezekano wa kuanza kufanya majaribio ya silaha za nyuklia ambazo inazo.

Kauli ya Russia kupitia kwa Rais wake, Vladimir Putin, inazidisha sintofahamu duniani, hasa kufuatia uamuzi wa Marekani na Nato, kutangaza waziwazi kuiunga mkono Ukraine, iliyovamiwa na Russia.

Putin amesema Marekani na washirika wake wa Ulaya, wanataka kuishinda Urusi katika Ukraine, kitu ambacho alisema lengo lao ni kuvichukua vinu vyake vya Nyuklia, kitu alichosema hakikubaliki.

Kwa miaka mingi sasa, tokea enzi za vita baridi, mikataba mbalimbali ilisainiwa ili kuhakikisha silaha za nyuklia hazifanyiwi majaribio na mataifa yanayozimiliki.

No comments