R KELLY SASA KUTOKA GEREZANI AKIWA MZEE WA MIAKA 80
Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya R&B duniani, R Kelly ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na picha zisizofaa za watoto na unyanyasaji wa kingono, sasa atatoka jela akiwa mzee wa umri wa miaka 80.
Robert Sylvester Kelly, alipewa hukumu hiyo na mahakama ya New York mwaka jana, lakini jana Alhamis mahakama ya Chicago imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la ulaghai wa kingono.
Hata hivyo, mwimbaji huyo wa kibao cha I Believe I Can Fly, ataumikia adhabu hizo kwa pamoja, hivyo kumfanya kuongeza mwaka mmoja tu gerezani baada ya hukumu ya New York.

Post a Comment