AJIRUSHA GHOROFANI NA KUFA KISA MZOZO WA KIMAPENZI

Visa wa watu kupoteza maisha kutokana na sababu za mapenzi vimezidi kuongezeka na safari hii, binti mwenye umri wa miaka 29 tu, amekatisha ndoto zake.

Brenda Kawira Gitonga, aliyekuwa akiishi na mpenziwe katika jengo lenye ghorofa nne, Kasarani jijini Nairobi, aliamua kujitoa uhai kikatili alipotoka cbumbani na kwenda ghorofa ya mwisho, kisha kujirusha chini, kufuatia mzozo wa muda mfupi wa kinyumba.

Baada ya kishindo kikubwa, majirani walimkimbiza katika Hospitali ya Uzima, ambako madaktari walithibitisha kuwa Brenda alikuwa ameshafariki.

No comments