MWILI WA RAIS WA ZAMANI WA BURKINA FASO WAZIKWA UPYA, MKEWE ASUSIA MAZISHI

Mwili wa Thomas Sankara, mwanamapinduzi kijana ambaye alikuwa Rais wa Burkina Faso umezikwa upya kutoka katika makaburi ya kawaida yaliyo nje kidogo ya mji mkuu, Ougadogou.

Sankara ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1983 akiwa kijana mdogo, aliuawa kwa kupigwa risasi yeye na wenzake 12 wakati wa mkutano, katika tukio lililopangwa na aliyekuwa Makamu wake, Blaise Compaore.



Mke wa kiongozi huyo aliyekuwa na cheo cha Kapteni jeshini wakati akitwaa madaraka, Miriam na watoto wake wawili walisusia mazishi hayo wakidai eneo alilozikwa, ambalo ndilo sehemu aliyouawa la Conseil de I'Entente halikuwa chaguo sahihi kwani linawakumbusha machungu.

Hata hivyo, wanafamilia wengine wa Sankara aliyependwa nchini humo, pamoja na wanafamilia wa wenzake 12 walihudhuria shughuli hiyo binafsi.

Kiongozi wa sasa wa Burkina Faso, Ibrahim Traore ndiye akiyeamuru mwaka jana kufanyika upya kwa mazishi ya kiongozi huyo aliyeuawa Oktoba 15, 1987.

No comments