QATAR YAPELEKA NYUMBA ZA KOMBE LA DUNIA UTURUKI

Serikali ya Qatar imepeleka nyumba za muda zilizotumika wakati wa fainali za kombe la dunia nchni Uturuki, ikiwa ni msaada wa makazi kwa waliothirika na tetemeko la ardhi lililoikumba taifa hilo pamoja na Syria.

Zaidi ya nyumba hizo 10,000 zinatarajiwa kupelwkwa nchini humo ambako hadi sasa watu wapatao milioni moja hawana makazi kufuatia tetemeko hilo linalikisiwa kusababisha vifo vya watu 40,000.

Shirika la mfuko wa maafa la Qatar, limesema tokea mwanzo wakati wa ujenzi wa makazi hayo ya muda, walifahamu kuna siku yatahitajika mahali.

No comments