MRADI BARABARA MWENDOKASI GONGO LA MBOTO KUKAMILIKA MACHI MWAKANI

,

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka kati ya Posta hadi Gongo la Mboto utakamilika Machi mwakani.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo wakati akifanya ukaguzi wa barabara hiyo akiwa ameongozana na watendaji kutoka Wakala wa Barabara TANROADS.

Aliwataka wakandarasi wa ujenzi huo, kampuni ya Sinohyro kufanyakazi kwa kiwango na muda ili kukidhi matakwa ya barabara hiyo, sambamba na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu kwa muda wa ujenzi.



Waziri aliitaka TANROADS kuhakikisha wanawaongoza vyema watumiaji wengine wa barabara wakati huu wa ujenzi ili kuhakiikisha makundi yote ya watumiaji yanaongozwa vyema ili kutotoa usumbufu wa wakandarasi.

Naye Meneja mradi, Injinia Barakaeli Mmari alisema mradi huo utakapokamilika utakuwa na vituo vikubwa viwili, vidogo 32 na daraja moja la watembea kwa miguu huku urefu wa barabara hiyo ukiwa ni km 23.


Naye Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam Injinia Senkuku alisema mamlaka yake imejipanga kuhakiisha ujenzi huo unaenda sambamba na programu ya kupendezesha jiji.



Jumla ya shilingi bilioni 236.7 zitatumika kujenga barabara hiyo yenye lengo la kupunguza msongamano wa magari kutoka katikati ya jiji kupitia barabara ya Nyerere.

No comments