MKATABA WA YANGA, HIER BADO WAMKERA ABBAS TARIMBA

Abbas Tarimba ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Sporpesa Tanzania, ameeleza namna mkataba wa Klabu ya Yanga na Kampuni ya Hier unavyoikera taasisi yake.

Katika mazungumzo na chombo kimoja cha habari jijini Dar es Salaam, alisema kitu pekee kinachowafanya wawe kimya wakati Yanga ikiiweka kampuni hiyo kifuani nwa jezi zao, ni kwa vile wana nia ya kuusaidia mpira wa Tanzania, vinginevyo hali ingekuwa mbaya.

Tarimba ambaye pia ni Mbunge wa Kinondoni kupitia CCM, alisema viongozi wa Yanga walifanya makosa makubwa kuingia mkataba huo na kosa zaidi ni kuwaambia wanachama na mashabiki kuwa wako sahihi.

Alisema kwa mujibu wa mkataba wao na klabu hiyo, kitendo cha Yanga kusaini mkataba mwingine haikuwa sawa, licha ya kuwa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika CAF haliruhusu kampuni za ubashiri kuzidhamini klabu kwa kuwa mdhamini mkuu wa michuano ya shirikisho, ni kampuni ya kubashiri pia.


No comments