ALIYEDAIWA KUWAPORA WALIOFARIKI AJALINI KOROGWE AKUTWA AMEJINYONGA MAHABUSU

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba, amethibitisha kwamba mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa kwa uporaji wa marehemu na majeruhi wa ajali iliyotokea Korogwe, iliyoua watu 20, amekutwa amejinyonga katika mahabusu.

Mtu huyo, ambaye rekodi zinaonyesha wakati akikamatwa nyumbani kwake alikutwa pamoja na vingine simu na nguo zilizokuwa zina damu, alikuwa miongoni mwa watuhumiwa nane waliokamatwa.

Ajali hiyo ilitokea wiki kadhaa zilizopita baada ya basi aina ya Coaster0 iliyokuwa imewabeba wanafamilia waliokuwa wakisafirisha mwili wa ndugu yao, kugongana na Fuso ambapo watu 20 walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

No comments