ESTHER BULAYA: NAKIPENDA CHAMA KIMOJA TU, CHADEMA

Esther Bulaya, mbunge wa zamani wa kuchaguliwa wa Jimbo la Bunda kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema yeye anakipenda chama kimoja tu, ambacho ni kile kolichompatia ubunge.

Esther, mmoja kati ya wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wa Chadema kwa kudaiwa kuingia bungeni msimu huu bila ridhaa ya chama hicho,alitajwa na chombo kimoja cha habari kuwa yeye na wenzake, wanajiandaa kujiunga na Chama Cha ACT-Wazalendo.

Lakini kupitia akaunti yake ya Twitter,akiwa ameliweka gazeti hilo, aliandika kuwa yeye anakipenda chama kimoja tu ambacho ni Chadema.

Esther na wenzake wamekata rufaa kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

No comments