BAADA YA MIAKA NANE, DK SLAA APANDA JUKWAA LA CHADEMA, ASEMA KIMEKOMAA KUSHIKA DOLA
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Wilbroad Slaa, amepanda katika jukwaa la chama hicho, miaka nane baada ya kujiondoa hapo mwaka 2015.
Akipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Karatu ambako aliwahi kuhudumu akiwa Mbunge, Dk Slaa alisema Chadema kwa sasa kimekomaa na kinaweza kushika dola.
Katika mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika leo katika Kata ya Rhotia mjini Karatu ukijadili kero mbalimbali za wananchi, balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Sweden alisema sera za afya za chama hicho ziliwahi kunvutia aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye aliifanya kuwa sera ya taifa.
Dk Slaa alijiweka pembeni na chama hicho akipinga kuteuliwa kwa Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzj wa 2015 na tokea wakati huo, hajawahi kupanda jukwaa la chama hicbo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu, Samwel Welwel alisema chama hicho hakijampokea kiongozi wake huyo wa zamani, bali alipewa nafasi ya kuwaalimia wananchi kwa kuwa aliwahi kuwa mbunge wao.

Post a Comment