KHADIJA KOPA ATAMANI NDOA TENA, ILA ATOA MASHARTI KWA ANAYEMTAKA
Khadija Omary Kopa, mwanamuziki mkongwe wa taarab, anatamani kuolewa tena, lakini ametoa masharti ambayo mashabiki wake mtandaoni wamemshambulia vibaya.
Khadija alisema masharti ya mwanaume anayemtaka ni lazima kwanza awe na uwezo wa kumtunza, lakini pia umri wake uwe wa miaka 50 na kuendelea.
Mwimbaji huyo ambaye umri wake unaelekea kuvuka miaka 60, alisema hana mpango wa kuwa na mwanaume wa umri mdogo maarufu kana kibenten.

Post a Comment