MELI ZA URUSI ZILIZOBEBA SILAHA ZA NYUKLIA ZAISOGELEA UKRAINE
Meli zilizobeba silaha za nyuklia, mali ya Urusi, zimeripotiwa kuisogelea Ukraine ambayo inapambana kiume kukabili uvamizi wa wababe wa kisoviet kwa zaidi ya mwaka sasa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la ujasusi la Norway, msafara wa meli hizo zilizobeba silaha za maangamizi, ni mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30.
Uamuzi huo wa Urusi kuzipeleka meli hizo, unadaiwa unafanywa ikiwa kama onyo kwa mataifa ya Magharibi ambayo yanaiunga mkono nchi hiyo ambayo ilikimega wakati dola kubwa la Sovieti liliposambaratika miongo kadhaa iliyopita.
Ukraine, imekuwa ikipokea misaada ya kijeshi na kibinadamu kutoka nchi za Magharibi na hivi karibuni ilipata msaada mkubwa wa vifaru vya kurusha makombora ya kujilinda kutoka Ujerumani.

Post a Comment