AHADI YA MILIONI TANO KILA GOLI YA RAIS SAMIA ITAENDELEA KWA YANGA, SIMBA

Ahadi ikiyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Klabu za Yanga na Simba, kuwamotisha kwa shilingi milioni 5 kwa kila goli watakalofunga, ni endelevu.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema, Rais Samia ataendelea kutoa kiasi hicho cha fedha kwa michezo yote ambayo timu hizo zinazoiwakilisha nchi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika itafunga bao.

Baada ya ahadi yake kwa mara ya kwanza, Simba walipoteza mchezo wao kwa kufungwa mabao 3-0 na Raja Cansablanca, lakini Yanga ikaibuka na ushindi usiotarajiwa wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Mechi zinazofuata wikiendi hii, Simba itasafiri kuelekeaa Uganda kutupa karata itayoamua hatma yake msimu huu dhidi ya Vipers wakati watani wao watakabiliana na wawakilishi wa Mali.

No comments