RUSSIA YAONYA VIFARU VYA UJERUMANI KUTUMIA NYUKLIA
Russia imeonya kuwa vifaru vya Ujerumani vinavyopelekwa Ukraine ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na Urusi kijeshi, huenda vikapachikwa vichwa vya makombora ya 'nyuklia'.
Ujerumani imekubali kuisaidia Ukraine vifaru hivyo vyenye uwezo wa kulinda mfumo wa ulinzi na kushambulia, kitendo ambacho kimeshutumiwa vikali na Ikulu ya Klemlin.
Konstantin Gavrilov, ambaye ni Mkuu wa Ujumbe wa Mazungumzo ya kusitisha vita, alisema makombora hayo yanayofahamika kama silver bullets yaliwahi kutumiwa na Marekani wakati wa vita vya Ghuba.
Yalitumika pia wakati wa mashambulizi ya majeshi ya Marekani na washirika wake huko Kosovo na Yugoslavia.
Russia ni moja ya mataifa yanayomiliki silaha za nyukilia na mara kadhaa imetishia kuzitumia kama Ulaya itaendelea kuisaidia kijeshi Ukraine, iliyoivamia miezi 11 iliyopita.

Post a Comment