DONE: HERSWIDA KOMBA KIDEDEA

Herswida Sines Komba (pichani, dakika chache kabla ya kutangazwa), ameibuka mshindi katika uchaguzi wa UVCCM wilaya ya Mbinga ambao ulikuwa na ushindani mkali.

Herswida aliyekuwa mwanamke pekee kugombea nafasi hiyo iliyokuwa na washindani wanne, alipata ushindi katika duru la pili la upigaji kura, kufuatia duru ya kwanza kutopata ushindi licha ya kuongoza.

Katika marudio hayo, mshindi huyo ambaye aliwataka vijana wa Mbinga kuvunja makundi wakati akitoa shukurani kwa wajumbe, alimshinda msshindani wake Isihaka Mohamed Rajabu.

Herswida anachukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ditram Lungu ambaye aliwaongoza vojana wa Mbinga kuanzia mwaka 2017-2022.

No comments