NGOMA NGUMU: DURU YA KWANZA HAKUNA MSHINDI
Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga umeshindwa kutoa mshindi katika raundi ya kwanza uliowashirikisha wagombea wanne.
Msimamizi wa uchaguzi huo aliwaambia wajumbe kuwa aliyeongoza katika zoezi hilo, Herswida Sines Komba alipata kura 261 kati ya wapiga kura 575. Ishindi huo haukumpa nafasi ya kutangazwa mshindi kwa kuwa kura zake hazikizidi nusu.
Kwa maana hiyo Herswida atapambanishwa na aliyemfuatia kwa kura, Isihalka Mohamed Rajabu aliyepata kura 138. Daniel Nkoma na John Mbawala wametupwa nje katika kinyang'anyiro hicho.
Pichani wagombea hao wawili wakiwa na namba zao za kupigiwa kura.

Post a Comment