PROFESA LUMUMBA AMTAKIA HERI YA KUZALIWA MAMA SAMIA

Profesa Patrick Loch Otieno (PLO) Lumumba, raia wa Kenya ambaye ni maarufu kwa mihadhara sehemu mbalimbali duniani, amemtumia salamu za kumtakia heri ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika video iliyotumwa kwenye akaunti ya Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, PLO Lumumba amesema Rais Samia ni kiongozi mpenda demokrasia na kwamba ana imani naye kwa ustawi wa watu wa Afrika Mashariki.

Amesema mwanamke huyo wa kwanza eneo hili kuchukua wadhifa huo, ana nia njema na Tanzania hivyo kuamini kuwa watanzania watamchagua tena katika uchaguzi ujao.

No comments