PEP, ARTETA USO KWA USO ENGLAND USIKU LEO
Marafiki wawili, waliopitia Barcelona na ambao sasa ni tishio katika Ligi Kuu England, Pep Gardiola na Mikel Arteta, leo watakutana wakiziongoza timu zao katika mchezo wa raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA.
Arteta atakwenda ugenini akiwa alama tano zaidi ya Pep kwenye ligi kuu, lakini hilo haliwezi kuwa jambo la kumpa nafasi ya ushindi, kwani licha ya kushika nafasi ya pili, bado Man City inatisha uwanjani.
Safu yake ya ushambuliaji ni kali, huku kinara wake wa mabao akiwa tayari ameshaingia nyavuni mara 25, idadi ya juu kabisa kuwahi kufikiwa na mshambuliaji mmoja kwa idadi ya mechi zilizochezwa hadi sasa.
Hata hivyo, Arsenal ya msimu huu ni tofauti kabisa, ikicheza soka la kasi kwa muda wote wa dakika tisini.
Mechi ya leo, ni moja kati ya tatu ambazo zinapaswa kuchezwa na timu hizo msimu huu. Bado hazijakutana mara mbili katika Ligi Kuu England msimu huu.

Post a Comment