BOSI WA MTANZANIA ALIYEFIA VITANI UKRAINE KUUAWA

Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa msituni, linalopigana kuisaidia Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, liitwalo Wagner, ambalo hivi karibuni lilimpoteza mpoganaji wake Mtanzania aliyeuawa vitani, yupo hatarini kuuawa.

Kwa mujibu wa taarifa za kiinteligensia kutoka Kremlin, makao makuu ya Russia, Yeugeny Prigozhin anawindwa kuuawa na majasusi wa CIA wakishirikiana na rais wa Ukraine.

Mbabe huyo wa vita ambaye anaitwa jina la utani la Mpishi wa Putin, anaongoza kundi lenye wapiganaji zaidi ya 50,000.

Katika picha, kiongozi huyo wa kundi linalotajwa kufanya uhalifu wa kivita na kukiuka haki za binadamu, anaonekana akimuhudumia Rais Vladimir Putin mwaka 2010 alipokuwa mpishi wake katika ikulu ya Klemlin.

No comments