KAPSCOM WAZEE WA INTERNET

Kampuni ya kizalendo ya Kapscom  

Africa Ltd  ya jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na ufungaji wa huduma za internet majumbani na maofisini, pamoja na CCTV Cameras Tanzania ina mpango wa kujitanua zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Henry Kapinga, ameiambia Ojuku Blog kuwa kwa sasa wapo zaidi jijini Dar es Salaam, lakini nia yao ni kujitanua zaidi nchini.

"Kwa sasa huduma zetu zipo Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Mwanza Arusha na Morogoro. Lengo la kampuni ni kutoa huduma hii nchi nzima, hasa kwa kutambua umuhimu wa huduma hi katika zama hizi za kidigitali.

"Mambo mengi hivi sasa yanaenda kidigitali, ni muhimu kwetu kusogea karibu zaidi na wananchi ili kukidhi mahitaji yao. Hii huduma siyo biashara, ni muhimu kulingana na wakati tulionao."

Kapinga, zaidi alisema wanafanya connectivity ya majumbani na maofisini kwa bei nafuu.

Kwa mawasiliano zaidi na kampuni hiyo yenye ofisi zake Victoria, barabara ya Bagamoyo, Makumbusho jijini Dar es Salaam katika jengo la iliyokuwa ofisi ya BMTL. Kwa mawasiliano zaidi, piga namba zao za simu 0713254563 | 0767254553 au Email: sales@kapscomafrica.co.tz


No comments