CHADEMA YAPULIZA KIPYENGA MWANZA
Siasa za ushindani zinaanza tena leo wakati chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema kitakapopuliza kipyenga cha uzinduzi wa mikutano ya hadhara baada ya kifungo kisicho rasmi cha miaka sita.
Uzinduzi huo unafanyika mida hii katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza vikiwahusisha viongozi wa juu wa chama hicho, chini ya Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.
Hali hiyo inakuja baada ya miaka sita ya marufuku ya mikutano ya hadhara ya kisiasa ya vyama vya siasa ukiondoa CCM iliyowekwa na Rais John Pombe Magufuli aliyeingia madarakani katika uchaguzi uliokuwa na ushindano mkali wa mwaka 2015, ambapo aloshindana na Edward Lowassa aliyepeperusha bendera ya Chadema.
Marufuku hiyo iliondolewa na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea ripoti ya kikosi kazi alochokiunda ili kuangalia maeneo ya kufanyiwa kazi kuweza kupata maridhiano ya kitaifa.
Rais Samia ameonyesha utayari wake katika siasa baada ya kukutana na viongozi wa vyama vyote na kusikiliza mawazo yao.
Maridhiano hayo ya kisiasa ndiyo yamepelekea wanasiasa wawili maarufu wa Chadema, Tundu Lissu na Godbless Lema kutaka kurejea nyumbani bà ada ya kuikimbia nchi kwa kile walichodai kuhofia usalama wao.
Locha ya kutokuwa katika uwanda sawa kisiaaa, vyama vya upinzani vilionyesha ushondani mkubwa katika uchaguzi iliopita, lakini kwa maajabu ya wengi, vyama hivyo vilikosa uwakilishi uliotarajiwa bungeni.
Baada ya Chadema kukata utepe leo, chama kingine kikubwa cha upinzani cha ACT Wazalendo nacho kinatarajiwa kufuata nyayo huku hali ikitegemewa kuwa hivyo pia kwa vyama vingine vidogo kama CUF, TLP, UDP, TADEA na vinginevyo.
Watu wengi wanatarajiwa kuwemo katika mkutano huo hasa baada ya chama hicho kupitia katika changamoto kadhaa, ikiwemo kuondoka kwa makada wake wakiwemo Joshua Nassari aliyejiunga na CCM, kufunguliwa kwa kesi ya uhujumu uchumi kwa Mwenyekiti wake wa Taifa na kufukuzwa kwa wanachama wao 19 ambao walijiteua na kuingia bungeni pasipo baraka za chama.

Post a Comment