WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU KUKOPESHWA BILIONI 67.6

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu
Hassan kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa imepanga kutoa shilingi Bil. 67.6
kama
Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu
kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo mapema leo Jijini Dodoma wakati
akikabidhi hundi ya shilingi 1,039,050,000 kwa vikundi 48 vya Halmashauri ya
Jiji la Dodoma.
Akikabidhi hundi hiyo Waziri Ummy amesema ni jukumu la kila
halmashauri kuhakikisha katika makusanyo yake ya ndani inatoa asilimia 10 kwa
ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu.
Pia Waziri Ummy amezitaka Halmashauri kutumia wataalam wake
kutoa elimu kwa vikundi vinavyotaka kukopo jinsi ya kutumia fedha hizo kwa
miradi yenye tija na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kurejesha haraka ili na
wengine waweze kunufaika.
Kwa upande wa mnufaika wa mikopo Bi.Gladius Jalee kutoka
kikundi cha Jeshi Kubwa kilichopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ameishukuru
Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza azma ya kuendelea kusimamia na
upatikanaji wa fedha za mikopo kwa kueleza kuwa kundi lao mpaka sasa wamefikia
hatua zuri ya ukopeshwaji kutokana na urejeshaji wao mzuri kuanzia kukopeshwa
kutoka shilingi milioni moja mpaka sasa kufikia kukopeshwa shilingi milioni
hamisini.

Post a Comment