NILIBONYEZWA MWILI MZIMA KUSAKWA MADAWA YA KULEVYA

FLORENCE Khambi, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Za Kulevya amesema kuwa aliposafiri
kuelekea nchini China, mamlaka za huko walimsachi kwa kiwango cha juu, ikiwa ni
pamoja na kubonyezwa kila sehemu ya mwili wake ili kusaka madawa ya kulevya
akidhaniwa ameyabeba.
Kamishna huyo amesema Watanzania
wanatajwa kuwa wanajihusisha zaidi na usafirishaji wa biashara ya dawa za
kulevya (Mapunda/Punda) hasa katika nchi za China, Hong Kong na Afrika Kusini.
Amesema kuwa alipata wakati mgumu wakati aliposafiri kuelekea
nchini China. Alifanyiwa ukaguzi wa hali ya juu sana.
"Nakumbuka wakati nilivyosafiri kwenda China kikazi
nilifanyiwa ukaguzi usio wa kawaida. Nilipekuliwa sana nilibonyezwa sana mwili
mzima"

Post a Comment