KIWANDA BUBU CHA SILAHA CHABAINIKA MSITUNI, MMOJA AKAMATWA
 
JESHI la Polisi Mkoani Tanga limesema wamebaini kiwanda
kimoja cha bunduki kilichokuwa misituni na kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa
kuhusika. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Safia Jongo amesema wamekamata
gobore 11.
Vitu vinavyodaiwa kukutwa kiwandani hapo ni vifaa vya kutengenezea
silaha ikiwemo mitambo ya kutengeneza gobore, 'trigger' na 'cocking handle'.

Post a Comment