AZIM DEWJI ANUNUA JEZI ZA MILIONI 20 NA KUZIGAWA KWA MASHABIKI WA TAIFA STARS

MFADHILI wa zamani wa Klabu ya
Simba, Azim Dewji amesema ameamua kutumia Tsh. milioni 20 kununua Tshirt
atakazozigawa kwa Vijana 2000 watakaoishabikia Timu ya Taifa ya Tanzania vs DRC
Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia.
Dewji ameyasema hayo leo na kuwataka Watanzania na Wadau wa
soka kushirikiana kwa pamoja kuiunga mkono Taifa Stars katika mchezo huo
utakaochezwa Novemba 11, 2021 na kuongeza kuwa atazikabidhi jezi hizo kwa TFF
ambapo watazigawa kwa vijana hao 2000 ambao wataenda uwanjani kushabikia, pia
atatoa tiketi 100 kwa ajili ya Wafanyakazi wake kwenda uwanjani.
"Tubadilike hii ni Timu yetu hatuombi pesa maana Waziri
Mkuu ameshakusanya pesa na amepata za kutosha na Mama naye amesema ana imani na
Timu, tumebakia sisi Wapenzi na Mashabiki kwamba lazima na sisi tuige na tufate
yale yaliyozungumzwa na Viongozi wetu, tunaomba siku ya alhamis tuwape ruhusa
Watanzania wakaishabikie Timu yetu"

Post a Comment