UJENZI YAFUZU KUINGIA NANE BORA SHIMIWI
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa kikapu waliovaa sare nyeusi wakikabiliana
vikali na Wapinzani wao Wizara ya Afya katika michezo ya Shimiwi, inayoendelea Mkoani
Morogoro.
Timu ya Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) imefuzu kuingia hatua ya nane bora ya mchezo wa
netball kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali
(SHIMIWI).
Timu hiyo imefuzu baada ya
kuwafunga wapinzani wao Wizara ya Afya kwa Magoli 22-14 na kujizolea ushindi wa kuingia nane bora .
Timu nyingine zilizotinga
hatua hiyo ya nane bora katika mchezo wa netiboli ni Hazina, Tamisemi,
Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
Wizara ya Elimu na Wizara Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Katika upande wa soka timu
za Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi, Tamisemi, Wizara ya Elimu,
RAS Mara na Wizara ya Katiba na Sheria nazo zimetinga hatua ya nane bora.
Aidha, katika mchezo wa kamba
wanawake timu nyingine zilizotinga hatua ya nane bora ni pamoja na RAS Iringa,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Hazina, Wizara ya Mifugo, Idara ya Mahakama, Tamisemi na Wizara
ya Mambo ya Ndani.
Hatua hizo zitaanza
kesho kwa mechi za netiboli timu ya Ujenzi itacheza na Wizara ya Sanaa,
Utamaduni na michezo, huku Hazina watakutana na Tamisemi, nayo Ofisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali watakutana na Wizara ya Katiba na Sheria.
Katika michezo ya robo fainali
kamba wanaume timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani watavutana na Wizara ya Maliasili
na Utalii; na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) watawakaribisha Idara
ya Mahakama.
Katika netiboli Sanaa,
Utamaduni na Michezo 22 vs Wizara ya Ardhi 18, Hazina 33 vs Wizara ya Maji 20,
Wizara ya Katiba na Sheria 19 vs Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA) 14, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 14, Wizara ya Elimu 39
vs Wizara ya Nishati 16, Tamisemi 57 vs RAS Ruvuma 12, Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 54 vs Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) 15.
Michuano hiyo inatarajia kufika
kilele tarehe 2 Novemba, ambapo washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali vikiwemo
vikombe, Medali na Vyeti.

Post a Comment