BIFU JIPYA KING ALI KIBA NA SHILOLE
KUNA dalili kubwa kuwa hali haiko sawa baina ya
wasanii wawili nyota hapa nchini, Ali Kiba na Zuwena maarufu kama Shilole.
Na sababu kubwa ni kitendo cha Shishi Baby kuhudhuria
sherehe za uzinduzi wa kazi mpya ya Ali Kiba pasipo mualiko kutoka kwa mkali
huyo wa muziki Tanzania.
Katika akaunti yake ya Instagram, Shilole ameandika. "Hapana jamani, kila siku nakosewa nikitaka
kuongea washauri wangu wanasema nikae kimya. HILI NIMEKOSEWA SANA NA SIWEZI
KUKAA KIMYA SASA MNANIONEA.
.
@officialikiba nakushukuru sana leo umeuthibitishia ulimwengu mambo
yafuatayo :
1. Una kiburi cha kishamba, unavimba na kupandisha mabega
katika namna isiyostahili. Huna utu ambao watu wako wanakupamba kwamba uko nao.
Sawa mimi na wewe hatuna mazoea (Hilo ni kweli kabisa), lakini mimi na wewe
tupo katika field moja. Ningeweza kuja kwenye shughuli yako kuonesha upendo tu
hata kama sijaalikwa, ungekuwa na utu, haikuwa na haja kwenda redio na kusema
“SIJAMUALIKA” : ili mimi nionekane nilivamia tu shughuli tu?. Shame on you Ali.
(ila kwa tabia zile za kwenda Marekani kuomba dada zako naniliu hushangazi)
.
2. Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu,
utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati
hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema
hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu? Kwa
hiyo hata Nasibu uliyeshindana naye miaka mingi akakugaragaza angeweza kualikwa
bila wewe kujua? (Nasibu humuwezi tusikudanganye). Wewe ndo msanii wetu wa
kimataifa? SIJAPENDA.
.
Kwa ufupi, sikuenda kwenye shughuli kama mvamizi. Nilialikwa,
nimescreenshot post yake na kupost hapo juu.
Shughuli ile ya hovyo hovyo na kupoa kama uji wa mngonjwa,
ilihitaji uwepo wangu. YEEES, Niliwasaidia kuchangamsha.
.
Katika mazingira ya sasa mimi hakuna lolote ninalofaidika kwa
kwenda kwenye shughuli ya Ali, sana sana nilienda kumuongezea followers.
.
Kama nahukumiwa, nihukumuni kwa kupenda shughuli za wenzangu.
Kila nikialikwa Zuwena mimi nakweenda kuonesha upendo. NA SITAACHA KUFANYA HIVYO
KWA SABABU YA WATU WALIOKOSA UTU NA SHUKRANI KAMA ALI.
.
Aah hasira zimeisha, njooni Shishi Food tule ubwabwa" - @officialshilole

Post a Comment