TONY KARAMA WA SIKINDE AFARIKI GHAFLA

Mpiga bass maarufu wa Orchestra
Mlimani Park "Sikinde Ngoma ya Ukae", Toni Karama amefariki ghafla
muda mfupi ulipita.
Mrisho ambaye ni mtoto wa
marehemu ameithibitishia Saluti5 kuwa Tony Karama amefariki dunia katika
hospital ya Regency alipokimbizwa baada ya kuzidiwa ghafla.
Kwa sasa mwili wa marehemu
umeshaenda kuhifadhiwa hospital ya Muhimbili na msiba uko Kariakoo mtaa Mafia
na Jangwani.
Mrisho ambaye anapatikana kwa namba
0656802070 amesema taratibu za mazishi zitatangazwa muda mfupi ujao.
Onyesho la mwisho la Tony
kushiriki na bendi yake ilikuwa Jumapili iliyopita katika ukumbi wa Loving
Tone, Temeke.
Tony alirejea nchini wiki chache
zilizopita akitokea Uturuki alipokwenda kushiriki matamasha ya muziki wa
kiasili.
Credit: Salute 5

Post a Comment