UJENZI YAICHARAZA RAS RUVUMA GOLI 33 KWA 21

 

Timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,(Sekta ya Ujenzi), yaibuka kidedea kwa goli 33 kwa 21 dhidi ya wapinzani wao Ofisi ya Katibu  tawala  Mkoawa Ruvuma ( RAS-RUVUMA).

Akizungumza katika mashindano ya Michezo ya Idara na wizara za Serikali (SHIMIWI), yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, kocha wa Timu ya Ujenzi Bi Mwamvita Mzee, amesema kuwa  katika kipindi cha kwanza Ujenzi iliongoza kwa magoli 14 huku RAS -RUVUMA ikiwa nyuma kwa mabao 12 na magoli yaliyosalia yalifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo 

Aidha, kocha huyo ameongeza kuwa wamejipanga vizuri  na wanatarajia kupata ushindi zaidi katika michuano mingine ya makundi huku wakiwa na kaulimbiu 'anayekuja na achapwe'.

Katika mchezo mwingine, Timu ya Mpira  wa pete  ya Sekta ya Ujenzi siku ya Jumamosi tarehe 23 mwezi huu  inatarajia kucheza   na Wizara ya Mambo ya nje katika  viwanja vya Jamhuri  Mkoani Morogoro. 

No comments