MEMBE AWAHI MAHAKAMANI KUSUBIRI HUKUMU YA MUSIBA

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje,
Bernard Membe amefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda Maalum ya Dar es
Salaam leo kwa ajili ya kusubiri hukumu dhidi ya Cyprian Musiba.
Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018
ambapo kesi hiyo iliitwa kwa mara ya kwanza Februari 26, 2019,
Katika kesi hiyo Membe amemshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti
la Tanzanite na Wachapishaji wa gazeti hilo ambapo anawadai Tsh. Bilioni 10 kwa
kumchafua, hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa mbele ya Jaji Joacquine De
Melo.
Musiba katika kesi hiyo anashtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa
anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea
wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo
ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Post a Comment