MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA, AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole
Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.
Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini
asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali
alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee
huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.
UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake
wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa
kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
WASIFU WA OLE SABAYA
Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma
Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John
University).
Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM
(UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya
Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.
Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani
Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano,
Hayati John Pombe Magufuli.
Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai
tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa
yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba
2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo
cha miaka 30 jela.

Post a Comment