ISIJE KUWA NI KUPIGA MABOMU MOCHUARI?

NIWE mkweli, jana Yanga imecheza vizuri pengine kuliko mara nyingi kwa miaka ya hivi karibuni. Yule Aucho ndiye alikuwa mchezaji wangu bora wa mchezo.
Baada ya matokeo hayo, watu wangu wa Yanga sasa wanasema Makolo na waje, tutawapiga Hamsa Alba. Ni kawaida ya mashabiki wa timu, hiyo ndiyo raha yao. Ila sisi mashabiki wa mpira, baada ya mchezo kuna maswali hujiuliza.
Mfano, Yanga imeshinda mechi nne mfululizo na sasa ipo kileleni kwa alama 12. Mechi ya kwanza iliifunga Kagera Sugar 1-0. Katika msimamo hadi muda huu, Kagera wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 8. Mchezo wao wa pili, Yanga iliifunga Geita Gold Mine kwa bao 1-0. Msimamo wa sasa unaonyesha Geita wapo nafasi ya 13 wakiwa na alama 2.
Mechi ya tatu, Yanga waliifunga KMC bao 1-0 na kwenye msimamo, vijana hao wa Kinondoni wapo nafasi ya 15 na alama zao mbili pia. Jana, Wananchi waliikwangua Azam 2-0. Waoka mikate wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo wakiwa na alama zao nne.
Tuje kwa wapinzani wao Lunyasi. Kabla ya mchezo wao wa leo dhidi ya Costo, Simba wapo nafasi ya tano wakiwa na alama 7 baada ya kucheza mechi tatu. Mechi yao ya kwanza ilikuwa 0-0 dhidi ya Biashara United. Katika msimamo wa leo, Biashara ipo nafasi ya tisa, ikiwa na alama 5 baada ya kucheza mechi nne.
Mechi yake ya pili, Simba ilishinda dhidi ya Dodoma Jiji kwa bao 1-0. Dodoma leo ipo nafasi ya pili, ikiwa na alama 10 baqda ya kucheza mechi tano. Mchezo wake wa tatu, Simba ilishinda dhidi ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0. Maafande hao hivi sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na alama tisa baada ya mechi nne.
Ukitazama mtiririko huo, katika mechi nne ambazo Yanga imeshinda, ni timu moja tu ambayo ipo ndani ya kumi bora katika msimamo, Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya nne. Zingine zilizobaki, Azam, Geita na KMC zipo katika nafasi ya kuanzia 11 kushuka chini.
Kwa upande wa Simba, katika mechi zake tatu ilizocheza, wapinzani wao wote wapo ndani ya 10 Bora. Aliyetoka naye sare, Biashara anakamata nafasi ya tisa wakati wawili aliowashinda, wanafukuzana na Yanga katika Tatu Bora!
My point is... ni kweli Yanga wako vizuri, lakini ni mapema sana kuanza kushangilia na kutabiri ubingwa kwa sababu timu ilizozishinda, kwa viwango vya hadi leo, ni duni sana tofauti na wale ambao wameshakutana na Simba

Post a Comment